SILABI YA KISWAHILI YA KIDATO CHA 5
Mukhtasari huu umeandikwa kwa kuzingatia
matokeo ya tathmini ya muhtasari wa 1976 iliyofanywa na Taasisi ya
ukuzaji Mitaala mwaka 1988. Mapendekezo hayo yalitokana na upimaji wa
uwezo wa wanafunzi na maoni ya
waalimu na wakaguzi.
Mada za mukhtasari huu zimepangwa kulingana
na vidato. Inashauriwa mada hizi zifundishwe kwa njia ya kuchanganya na si kwa
kufuata mtiririko wa mada uliomo kwenye muhtasari huu. Kwa mfano, katika wiki
moja, mwalimu anaweza kufundisha vipengele
vya fasihi simulizi kwenye kipindi kimoja, vya sarufi kipindi kingine na vya
utungaji katika vipindi vingine.
Mwalimu
anashauriwa kuzingatia yafuatayo
- Pamoja
na njia/mbinu za kufundishia zilizoandikwa humu, mwalimu abuni njia nyingine
kulingana na uwezo na vionjo vya
wanafunzi wake.
- Atengeneze
na kutumia vifaa vya kufundishia kulingana na mahitaji ya wanafunzi wake.
- Ajielemishe
kwa kusoma maandiko mbalimbali yanayochapishwa kila wakati.
- Awe
mfano mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiswahili fasaha.
- Orodha
ya vitabu vya kufundishia Kiswahili itakuwa ikitolewa na Wizara ya Elimu kila
baada ya muda maalum.
- Muhtasari
huu unahitaji vipindi kumi na viwili kwa wiki.
Malengo ya
kufundisha kiswahili katika shule za Sekondari
Mafunzo ya Kiswahili katika shule za Sekondari yanakusudiwa
kuwawezesha wanafunzi
- Kutumia
Kiswahili kwa ufasaha katika fani zote za maisha
- Kuhakiki
kazi za fasihi ya Kiswahili
- Kujenga
tabia ya udadisi katika masuala ya lugha ya Kiswahili
- Kuelewa
kuwa Kiswahili ni sehemu muhimu ya Utamaduni wa Tanzania
Malengo ya Kidato
cha Tano
Wanafunzi waweze:
- Kufafanua
chimbuko la Kiswahili
- Kueleza
ukuaji na ueneaji wa kiswahili
- Kufafanua
nadharia ya fasihi
- Kujadili
dhima ya udhamini wa kifasihi
- Kujadili
nadharia ya uhakiki wa kifasihi
- Kufafanua
tanzu za fasihi simulizi
- Kujadili
mbinu za kifani katika fasihi simulizi
- Kujadili
ukuaji wa fasihi simulizi
- Kujadili
uhifadhi wa fasihi simulizi
- Kuhakiki
fasihi simulizi
- Kutunga
kazi za fasihi simulizi
- Kufafanua
tanzu za fasihi andishi
- Kujadili
mbinu za kifani
katika fasihi andishi
- Kujadili
ukuaji wa fasihi andishi
- Kuhakiki
kasi za fasihi andishi
- Kutathmini
mitazamo ya wanafasihi
- Kutunga
kazi za fasihi andishi
- Kutambua
kauli ya Kiswahili
- Kubainisha
virai na vishazi
- Kueleza
muundo wa ngeli
- Kuchanganua
sentesi kwa njia ya mishale na
maelezo
- Kujibu
maswali ya ufahamu
- Kujadili
mada anuwai
- Kutumia
taratibu za uandishi
- Kutumia
lafudhi ya Kiswahili
- Kuandika
insha, simu, mialiko na barua
- Kutambua
mitindo anuai katika kuzungumza na kuandika
- Kutambua
mbinu za kifani katika kuzungumza na kuandika
- Kueleza
dhima za mbinu za kifani
- Kutathmini
matumizi ya semi na tamadhali
- Kutambua
makosa ya kisarufi na kimantiki
- Kusahihisha
makosa ya kisarufi na kimantiki
MADA
- HISTORIA
YA KISWAHILI
- FASIHI
KWA JUMLA
- FASIHI
SIMULIZI
- FASIHI
ANDISHI
- SARUFI
- UFAHAMU
NA UFUPISHO
- UTUNGAJI
- UTUMIZI
WA LUGHA