SILABI YA KISWAHILI YA KIDATO CHA 6
Mukhtasari huu umeandikwa kwa kuzingatia
matokeo ya tathmini ya muhtasari wa 1976 iliyofanywa na Taasisi ya
ukuzaji Mitaala mwaka 1988. Mapendekezo hayo yalitokana na upimaji wa
uwezo wa wanafunzi na maoni ya
waalimu na wakaguzi.
Mada za mukhtasari huu zimepangwa kulingana
na vidato. Inashauriwa mada hizi zifundishwe kwa njia ya kuchanganya na si kwa
kufuata mtiririko wa mada uliomo kwenye muhtasari huu. Kwa mfano, katika wiki
moja, mwalimu anaweza kufundisha vipengele
vya fasihi simulizi kwenye kipindi kimoja, vya sarufi kipindi kingine na vya
utungaji katika vipindi vingine.
Mwalimu
anashauriwa kuzingatia yafuatayo
- Pamoja
na njia/mbinu za kufundishia zilizoandikwa humu, mwalimu abuni njia nyingine
kulingana na uwezo na vionjo vya
wanafunzi wake.
- Atengeneze
na kutumia vifaa vya kufundishia kulingana na mahitaji ya wanafunzi wake.
- Ajielemishe
kwa kusoma maandiko mbalimbali yanayochapishwa kila wakati.
- Awe
mfano mzuri wa kuzungumza na kuandika Kiswahili fasaha.
- Orodha
ya vitabu vya kufundishia Kiswahili itakuwa ikitolewa na Wizara ya Elimu kila
baada ya muda maalum.
- Muhtasari
huu unahitaji vipindi kumi na viwili kwa wiki.
Malengo ya
kufundisha kiswahili katika shule za Sekondari
Mafunzo ya Kiswahili katika shule za Sekondari yanakusudiwa
kuwawezesha wanafunzi
- Kutumia
Kiswahili kwa ufasaha katika fani zote za maisha
- Kuhakiki
kazi za fasihi ya Kiswahili
- Kujenga
tabia ya udadisi katika masuala ya lugha ya Kiswahili
- Kuelewa
kuwa Kiswahili ni sehemu muhimu ya Utamaduni wa Tanzania
Malengo ya Kidato cha Sita
Wanafunzi waweze
- Kufafanua
dhima ya vyombo vya habari katika
kukuza na kueneza kiswahili
- Kueleza
maana na matumizi ya pijini, lahaja
na kreole
- Kueleza
maana na matumizi ya lugha ya kwanza,
ya pili, rasmi
na ya taifa
- Kujadili
mbinu za kifani katik afsihi simulizi
- Kujadili
ukuaji wa fasihi simulizi
- Kujadili
uhifadhi wa fasihi simulizi
- Kuhakiki
kazi za fasihi simulizi
- Kutunga
kazi za fasihi simulizi
- Kuhakiki
kazi za fasihi andishi
- Kufafanua
maana matumizi na mipaka ya uhuru wa mwandishi
- Kuhakiki
misimamo ya waandishi
- Kufafanua
aina za maneno
- Kufafanua
matumizi ya ngeli
- Kuchanganua
sentesi kwa njia za matawi, majedwali, maelezo na mishale.
- Kujibu
mswali ya ufahamu
- Kubainisha
mawazo makuu
- Kutathmini
habari
- Kujenga
hoja
- Kuandika
insha, risala, hotuba, matangazo na barua
- Kutambua
mitindo ya uzungumzaji na uandishi
- Kutumia
sanaa ya uzungumzaji hadharani
- Kuhakiki
fani katika fasihi
- Kutambua
makosa ya kisarufi na kuyasahihisha
- Kujadili
dhima ya rejesta katika lugha.
MADA
- HISTORIA
YA KISWAHILI
- FASIHI
SIMULIZI
- FASIHI
ANDISHI
- SARUFI
- UFAHAMU
NA U FUPISHO
- UTUNGAJI
- UTUMIZI
WA LUGHA